Gallery
Basi ikawa akaandaa ile mboga mwanzo hadi mwisho akiwa mtupu vilevile bila kujali. Muda mrefu alisimama, mara kadhaa alikaa kwenye kigoda cha plastiki, na mara kadhaa aliinama kwa muda akikatakata ama kuchanganyachanganya vitu. Kijiupepo kwa mbali kilipompuliza sehemu zake za mwili ambazo kwa kawaida huwa ndani ya nguo wakati wote, alihisi raha ya ajabu na msisimko zaidi. Alikuwa peke yake… alijiachia na kujisahau.
Walipotoka bafuni wote walirudi tena jikoni kukamilisha maandalizi ya chakula. Mara hii Da’Jesca akiwa ndani ya kanga moja na mumewe taulo kubwa jeupe. Wote bila nguo nyingine yoyote ndani. Mapishi yalipokamilika kwa pamoja waliandika meza na kuketi kwa mlo, huku mwanaume akiwa na hakika kabisa chakula kilichoandaliwa kitakuwa kitamu ile mbaya, bila kujali ni chakula gani.
Ni vyema tujiulize, je ni kiasi gani cha fedha tunatumia kila mwaka kununua nguo mpya, viatu vya gharama, vipodozi na mikoba? Bila shaka ni gharama kubwa lakini je, kuna gharama gani tunatumia kujenga furaha na amani ndani yetu? Jibu ni rahisi tu furaha na amani ni wewe mwenyewe pasipo gharama yoyote ile. Maswali haya yatakufanya wewe kama mwanamke mpenda urembo kupata njia thabiti za kuongeza urembo.






